HEMA YA MUSA
MWOKOZI ALIYEPO DAIMA Kijana mmoja wa Kiskoti, kwa jina Petro, alipopotea katika nyika yenye majani mengi usiku mmoja uliokuwa na Je! isingekuwa ni ajabu kwetu sisi 1. Kwenda Kwa Yesu Bila Kizuizi Amini usiamini, sisi tunaweza kwenda karibu Kristo anapenda kujenga uhusiano wake na kila mmoja wetu. Hii ndiyo sababu moja iliyomfanya aondoke duniani humu ili kwenda mbinguni kufanya huduma ya pekee ambayo ingemwezesha kuja karibu na kila mmoja wetu kila siku. Kwa sababu Yesu hajafungwa mahali pamoja Je, ni ahadi gani ya kutia moyo aliyoitoa Yesu kabla hajapaa juu kwenda mbinguni? Je, Kristo anafanya kazi gani kule mbinguni ambayo inafanya uwezekano uwepo kwa yeye kuwa "pamoja nanyi siku zote?" Zingatia ahadi hizi zinazotolewa kwetu tunapokuwa na Yesu Je, Yesu anakaa mahali gani kule mbinguni? Kristo aliye hai-mmoja anayetuelewa sisi-ni mwakilishi wetu kila mmoja binafsi katika kiti kile cha enzi "mkono wa kuume wa Mungu." Ni kwa jinsi gani maisha ya Yesu yalimwandaa kuwa Kuhani wetu? "Ndugu" yetu aliyeshiriki katika ubinadamu wetu, na ambaye "alijaribiwa" kama sisi tunavyojaribiwa, hivi sasa yeye ni Kuhani wetu Mkuu ameketi upande wa kulia wa Mungu, "Alifanywa kama" sisi, anajua yale tunayoyapitia. Amepata kuwa na njaa, kiu, majaribu, na kuchoka sana kiasi cha kuishiwa nguvu. Alijisikia kwamba alikuwa na haja ya kuhurumiwa na kueweleka. Lakini zaidi ya hayo yote, Yesu anazo sifa za kuwa Kuhani wetu Mkuu kwa sababu yeye alikufa ili "kufanya upatanisho" kwa ajili ya dhambi zetu. Alilipa gharama yote ya dhambi zetu kwa kufa badala yetu sisi. Hii ndiyo Injili, yaani, Habari Njema kwa wanadamu wote kila mahali na kwa wakati wote. Mmojawapo wa Wakurugenzi wa Shule yetu ya Biblia anatusimulia kisa hiki kilichompata akisema "Binti yetu mdogo kabisa alipokuwa na umri wa miaka mitatu, alijibana kidole chake katika kiti cha kukunjwa, na kuuvunjavunja mfupa wake. Tulipomkimbiza kumpeleka kwa daktari, kilio chake kikali kutokana na maumivu yake kiliturarua kweli mioyo yetu. Tena kikamgusa mtoto wetu wa miaka mitano kwa njia ya pekee. Sitaweza kusahau maneno yake aliyosema baada ya daktari kumshughulikia dada yake aliyejeruhiwa. Binti yule akalia kwa kwikwi, na kusema, 'Baba, natamani kingekuwa ni kidole changu mimi!" Wanadamu wote waliposetwa na dhambi na kuhukumiwa kufa milele, Yesu alisema, "Baba, natamani ningekuwa mimi." Naye baba akampa Yesu kile alichotamani pale msalabani. Mwokozi wetu amepitia kila aina ya maumivu makali ambayo kwayo sisi tuliteseka - na zaidi ya hayo! 2. Injili Katika Agano Wana wa Israeli walipopiga kambi yao chini ya Mlima Sinai, Mungu alimwagiza Musa kujenga patakatifu ambapo paliweza kusafirishwa toka mahali hata mahali kwa ajili ya ibada "kama mfano wake, ulioonyeshwa [kwako Musa] mlimani "(Kutoka 25:40). Karibu miaka 500 baadaye, Hekalu kuu la mawe la mfalme Sulemani lilijengwa ili kuchukua mahali pa hema takatifu lililokuwa likichukuliwa huku na huku. Na hekalu lile lililjengwa kwa mfano ule ule kabisa kama lilivyojengwa hema takatifu lililokuwa linachukuliwa huku na huku. 3. Huduma Ya Yesu Kwetu Imefunuliwa Katika Patakatifu Patakatifu na huduma zake hufunua kile anachofanya Yesu sasa katika hekalu la mbinguni, na anachofanya sasa hapa duniani ili kututayarisha na kutuongoza kila mmoja wetu katika maisha yetu ya kila siku. Kwa kuwa patakatifu pale pa duniani palijengwa kwa mfano wa hekalu la mbinguni, basi, panaakisi patakatifu pa mbinguni ambako Kristo anahudumu sasa. Kutoka 25-40 huelezea habari za huduma ile na taratibu zake za kafara ya patakatifu pale pa jangwani kwa kinagaubaga sana. Muhtasari mfupi wa vyombo vya patakatifu huonekana katika Agano Jipya: Hema hilo takatifu lilikuwa na vyumba viwili, yaani, Patakatifu, na Patakatifu pa Patakatifu. Ua uliwekwa mbele ya pataktifu. Katika ua ule ilisimama madhabahu ya shaba nyeupe ambayo juu yake makuhani walitoa dhabihu zao, na birika la maji walimonawa. Dhabihu zilizotolewa juu ya madhabahu ile ya shaba nyeupe zilikuwa mfano wa Yesu, ambaye, kwa njia ya kifo chake msalabani alikuwa ndiye yule "Mwana-kondoo wa Mungu, aichukuaye dhambi ya ulimwengu! (Yohana 1:29). Mwenye dhambi aliyetubu alipokuja na dhabihu yake kwenye madhabahu ile na kuziungama dhambi zake, alipokea msamaha na utakaso. Vile vile mwenye dhambi leo anapata msamaha na utakaso kwa njia ya damu yake Yesu (1 Yohana 1:9). Katika chumba kile cha kwanza, au Patakatifu, kile kinara cha taa saba kiliwaka daima, kikimwakilisha Yesu ambaye ni "Nuru ya ulimwengu" inayowaka daima (Yohana 8:12). Meza ya mikate iliyowekwa wakfu ilimwakilisha yeye ambaye ni "Mkate wa Uzima" ambaye daima yupo kukidhi njaa yetu ya kimwili na kiroho (Yohana 6:35). Ile madhabahu ya dhahabu ya kufukizia uvumba iliwakilisha huduma ya Yesu ya uombezi anayofanya kwa ajili yetu mbele za Mungu (Ufunuo 8:3,4). Chumba cha pili, au Patakatifu pa Patakatifu, palikuwa na sanduku la agano lililofunikwa na dhahabu pande zote. Liliwakilisha kiti cha enzi cha Mungu. Kifuniko chake cha upatanisho, au kiti cha Rehema, kiliwakilisha uombezi wa Kristo, Kuhani wetu Mkuu, akiwaombea wanadamu wenye dhambi ambao wameivunja sheria ya Mungu ya Maadili [Amri Kuu]. zile mbao mbili za mawe ambazo juu yake Mungu aliandika Amri Kumi zilihifadhiwa chini ya kile kiti cha rehema. Makerubi wale wawili wa dhahabu wenye utukufu waliinamia kile kiti cha rehema kutoka katika kila mwisho wa lile sanduku. Nuru tukufu iliangaza katikati ya wale makerubi wawili, hiyo ikiwa ni ishara ya kuwako kwake Mungu mwenyewe. Pazia lilipaficha pale Patakatifu ili pasionekane na watu wakati makuhani walipokuwa wakiwahudumia katika ule ua. Pazia la pili mbele ya Patakatifu pa Patakatifu lilikikinga kile chumba cha ndani kisionekane na makuhani walioingia katika chumba kile cha kwanza cha Patakatifu. Yesu alipokufa pale msalabani, je, ni kitu gani kilitokea kwa pazia lile? Patakatifu pa Patakatifu paliachwa wazi Yesu alipokufa. Baada ya kifo cha Yesu, hakuna pazia liwalo lote lote liwezalo kuwepo kati ya Mungu Mtakatifu na muumini aliye mnyofu wa moyo; Yesu, Kuhani wetu Mkuu, anatukaribisha na kutuingiza kabisa mbele za Mungu (Waebrania 10:19-22). Tunayo njia ya kukifikia chumba kile ambamo kimo kiti cha enzi cha Mungu kwa kuwa Yesu ni Kuhani wetu Mkuu aliye mkono wa kulia wa Mungu. Yesu ndiye anayetuwezesha sisi kuja mbele za Mungu - yaani, hadi ndani ya ule moyo wa upendo wa Baba. Basi "na tukaribie." 4. Ufunuo Wa Kristo Akifa Kutuokoa Kama palivyotumika pale patakatifu pa kidunia Kitabu kile cha Mambo ya Walawi cha Agano Katika zile huduma za kila siku makuhani wale waliotoa dhabihu kwa ajili ya mtu mmoja binafsi na kwa ajili ya mkutano mzima. Mtu ye yote alipotenda dhambi, alitakiwa kuleta mnyama asiye na waa lolote 5. Kwa Nini Damu? "Pasipo kumwaga damu hakuna msamaha" (Waebrania 9:22). Kile kilichotokea katika patakatifu pale pa Agano Yesu alipomwaga damu yake kutoka katika msalaba ule, alikuwa anatoa sadaka ya maisha yake makamilifu ya utii kuwa badala ya kushindwa kwetu kwingi. Baba na Mwana walipotenganishwa kwa nguvu pale Kalvari, Baba aligeuka na kuangalia kwingine kwa utungu na Mwanawe alikufa kutokana na moyo wake uliopasuka. Mungu Mwana aliingia katika historia yetu na kuchukua mwilini mwake athari kamili za dhambi zetu na kuonyesha wazi jinsi utendaji wa mabaya unavyoleta maafa ya kusikitisha kweli kweli. Hapo ndipo angeweza kuwasamehe wenye dhambi bila ya kuihafifisha dhambi. Kristo alifanya "amani kwa damu yake iliyomwagika pale msalabani" (Wakolosai 1:20). 6. Ufunuo Wa Yesu Akiishi Kutuokoa Je! ni kazi gani anayofanya Yesu siku-kwa-siku katika hekalu lile la mbinguni? Yesu sasa "yu hai' ili kutoa damu yake, yaani, kafara yake, kwa ajili yetu. Sasa yeye anafanya kazi kwa bidii nyingi ili kumwokoa kila mwanadamu kutoka katika dhambi iletayo mauti. Wengine kwa kuelewa vibaya wanadhani kwamba Yesu, akiwa kama Mwombezi wetu, yuko kule mbinguni kwa madhumuni ya kumsihi Kama Kuhani wetu Mkuu, Kristo pia anawasihi Mungu aliyatoa maisha yake na kufa kwa ajili ya kila mwanadamu aliyepata kuishi katika dunia hii. Na sasa, yeye akiwa Kuhani Mkuu au Mpatanishi, "yu hai siku zote" ili kuwaongoza watu wakikubali kifo chake kwa ajili ya dhambi zao. Wanadamu hawatapotea kwa kuwa wao ni wenye dhambi, bali kwa sababu wanakataa kupokea msamaha ambao Yesu anawapa. Dhambi iliharibu uhusiano wa karibu Kifo chake Kristo kilichotolewa | |
0 commentaires:
Enregistrer un commentaire
Abonnement Publier les commentaires [Atom]
<< Accueil